Benki ya Dunia imepunguza makadirio ya ongezeko la pato la taifa la Rwanda hadi asilimia 5.8 kutoka asilimia 6.2. Hatua hiyo inatokana na Benki hiyo kukadiria kuwa, maafa ya mafuriko yaliyotokea mwezi Aprili na Mei nchini Rwanda yatasababisha kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.