Xi atoa wito wa kuwa na maendeleo mapya katika utawala wa Sichuan kwenye ziara yake ya ukaguzi mkoani humo
2023-07-31 10:09:14| CRI

Rais wa China Xi Jinping, amefanya ziara ya ukaguzi mkoani Sichuan kusini magharibi mwa China.

Alisisitiza kwamba ili kuelewa kikamilifu na kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, inapaswa  kutekeleza kazi kuu ya Chama katika safari mpya ya zama mpya , na kufahamu kwa uthabiti uhusiano kati ya mambo ya kisasa ya China na mahitaji yake muhimu. Vilevile amebainisha kuwa ni muhimu kufanya maendeleo ya hali ya juu kama kipaumbele cha kwanza, na kutumia  dhana mpya ya maendeleo, kuunda muundo mpya wa maendeleo na  kuhimiza ustawi wa pamoja katika mchakato mzima wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi.Aidha ameitaka Sichuan kuelewa vizuri nafasi yake ya kimkakati na jukumu lake katika maendeleo ya jumla ya nchi, na  kufanya kazi yake kwa kufuata hali yake halisi,   na kubainisha wazi mawazo yake juu ya maendeleo na malengo yake makuu . Kwa maana hiyo, mkoa huo unapaswa kutumia kikamilifu uwezo wake ili kupata mafankio mapya katika   kuondoa mapungufu yake, kuboresha uwezo wake wa uvumbuzi wa kisayansi na teknolojia, kujenga mfumo wa viwanda vya kisasa, kuhimiza ustawishaji wa vijiji , na kuimarisha usimamizi wa mazingira ya ikolojia ili maendeleo mapya yapatikane katika utawala na ustawishaji  wa Sichuan katika zama mpya .