China yatoa maabara ya kisasa ya kupima alama za vidole kwa Malawi
2023-07-31 11:53:56| cri

Serikali ya China imetoa msaada wa maabara ya kisasa ya upimaji wa alama za vidole yenye thamani ya dola za kimarekani 143,000 kwa Jeshi la Polisi la Malawi, ili kuboresha utekelezaji wa sheria nchini humo.

Akipokea msaada huo, Inspekta Jenerali wa Polisi wa Malawi, Merlyn Yolamu ameishukuru serikali ya China kwa kuliunga mkono jeshi la polisi la nchi hiyo, akisema matumizi ya maabara hiyo yatasaidia ufanisi wa operesheni za polisi, na kuleta manufaa kwa taifa kwa ujumla.

Naye Balozi wa China nchini Malawi, Long Zhou amesema, maabara hiyo inatarajiwa kuchukua nafasi muhimu katika upelelezi wa kesi za kihalifu nchini Malawi, hivyo kuongeza ufanisi na matokeo mazuri ya operesheni za polisi.