Hospitali ya Muhimbili nchini Tanzania imekidhi vigezo AFCON 2027
2023-07-31 11:54:33| cri

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) nchini Tanzania imefuzu kuwa na uwezo wa kushughulikia dharura za kiafya zinazoweza kujitokeza katika michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) endapo Afrika Mashariki itapewa ridhaa ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

Haya yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania, Saidi Yakub ambaye aliambatana na jopo la wakaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waliopo nchini kukagua miundombinu muhimu ikiwemo viwanja vya michezo, hoteli, uwanja wa ndege na hospitali.

Amesema ukaguzi unakwenda vizuri na kwamba Muhimbili imekidhi vigezo vilivyotakiwa na zinasubiriwa tu baadhi ya nyaraka ambazo wakaguzi hao wameziomba.