Madaktari wa China watoa huduma za matibabu bure nchini Ethiopia
2023-07-31 10:15:09| CRI

Madaktari wa China Jumapili walitoa huduma zinazohitajika kwa wafanyakazi wapatao 240 katika Eneo la Viwanda la Mashariki (EIZ),  umbali wa kilomita 40 kusini mwa Addis Ababa, Ethiopia.

Jumla ya madaktari 36 kutoka  timu ya 24 ya madaktari wa China nchini Ethiopia, Timu ya 9 ya Madaktari wa Jeshi la Ukombozi la Umma la  China nchini Ethiopia, pamoja na Hospitali Kuu ya Njia ya Hariri ya Addis Ababa iliyowekezwa na China walishiriki katika shughuli hiyo. Matibabu ya bure yalitolewa chini ya kaulimbiu "Tufuatilie Afya ya Wafanyakazi wa Ethiopia."

Mtafsiri anayefanya kazi katika kampuni ya usindikaji wa chakula ya EIZ,    Tariku Mamo amesema kuwa kwa muda mrefu, amesumbuliwa na maumivu ya goti na sasa amepata matibabu kutoka kwa madaktari wa China kwa msaada wa huduma ya picha, na kushauriwa jinsi ya kufanya ili kupunguza maumivu. Mamo ameshukuru sana kwa huduma na kujitolea kwao katika kuwasaidia kulinda afya zao, akisema, jambo hilo lina maana kubwa kwao.