Mlipuko wa mabomu watokea kwenye mikusanyiko ya kisiasa Pakistan
2023-07-31 10:08:00| CRI

Msemaji wa shirika la uokoaji la Pakistan Bilal Faizi alisema, mlipuko wa mabomu ulitokea Jumapili kwenye mikusanyiko ya kisiasa huko eneo la Bajaur, kaskazini magharibi mwa Pakistan, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 10 na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.

Msemaji huyo alisema mlipuko huo ulishambulia mikusanyiko ya kisiasa ya chama cha Jamiat Ulema-e-Islam-Fazl (JUI-F) iliyoko karibu na eneo la Shanday Mor kwenye barabara ya Munda Khar huko Bajaur, sehemu ambayo iko mkoani Khyber Pakhtunkhwa, kaskazini magharibi mwa Pakistan unaopakana na Afghanistan. Idadi ya vifo vya watu inaweza kuongezeka kutokana na majeruhi wasiopungua 15 walioko katika hali mahututi.

Hadi sasa, hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na mlipuko huo.