Michezo ya 31 ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya FISU ya Chengdu 2021 (Chengdu Universiade) iling’oa nanga rasmi hii tarehe 28. Michezo hii iliyokuwa ifanyike miaka miwili iliyopita ila ikahairishwa kutokana na janga la COVID-19, imewaleta pamoja wachezaji na wanariadha kutoka nchi 170 na maeneo mbalimbali kote duniani. Miongoni mwa wachezaji hao ni wanafunzi watatu kutoka Kenya. Mwanahabri wetu Tom Wanjala anazungumza na mwanariadha Kelvin Kimtai ambaye tayari yuko China na anajiandaa kushiriki kwenye mbio za mita 10,000 na zile za kilomita 21.