Kenya na Uganda zinakusanya kwa pamoja rasilimali ili kumaliza awamu ya mwisho ya ujenzi wa reli ya SGR kati ya Mombasa, Nairobi, Naivasha, Kisumu, Malaba na Kampala.
Hayo yamesemwa na Mawaziri wa Uchukuzi wa nchi hizo mbili waliokutana mjini Mombasa, Kenya, ijumaa iliyopita. Katika taarifa yao ya pamoja, mawaziri hao wamesema, kwa kushirikiana pamoja na kupata ufadhili zaidi unaohitajika, utekelezaji wa awamu ya mwisho wa reli hiyo ya SGR utamalizika kabla ya muda uliopangwa.
Mwezi Novemba mwaka 2016, Kenya na Uganda zilisaini makubaliano ya pande mbili ya operesheni ya pamoja ya reli ya SGR ya kati ya Mombasa na Kampala, makubaliano yaliyothibitishwa mwaka 2017 mwezi Februari na Mawaziri wa Fedha wa nchi hizo.