Umoja wa Afrika walitaka jeshi la Niger kurejesha utawala wa kikatiba ndani ya siku 15
2023-07-31 23:18:16| cri

Kamati ya Amani na Usalama ya Umoja wa Afrika (AUPSC) imelitaka jeshi la Niger kurejesha utawala wa kikatiba ndani ya siku 15 kuanzia jumamosi iliyopita.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano wa Kamati hiyo uliofanyika Ijumaa kuhusu mapinduzi ya nchini Niger, na kuwataka maofisa wa jeshi kurejea kambini na kurejesha utawala wa kikatiba.

Kamati hiyo pia imepongeza juhudi zinazofanywa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kusuluhisha mgogoro unaoendelea nchini Niger.

Jumatano iliyopita, wanajeshi wa nchini Niger walitangaza kupindua serikali inayoongozwa na rais Mohamed Bazoum aliyeingia madarakani mwaka 2021 baada ya kushinda uchaguzi wa rais.