Waziri wa Maendeleo ya Nishati wa Zimbabwe, Soda Zhemu, amesema tatizo la mgao wa muda mrefu wa umeme nchini humo kwa sasa ni historia, na hii inatokana na kukamilika kwa upanuzi wa kitengo cha 7 na cha 8 katika Kituo cha Uzalishaji wa Umeme kwa Joto la Ardhini cha Hwange.
Waziri huyo amesema, kituo hicho kitafunguliwa rasmi alhamis wiki hii na rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, na kuongeza kuwa, taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kuwa nchi hiyo itarejea katika mgao wa umeme si za kweli, kwa kuwa nchi hiyo kwa sasa ina uhakika wa upatikanaji wa umeme.
Mradi huo umetekelezwa na kampuni ya Sinohydro ya China, na umeongeza megawati 600 katika Kituo cha Uzalishaji Umeme cha Hwange.