Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amekemea mawimbi ya hivi karibuni ya mabadiliko ya serikali barani Afrika yaendayo kinyume na katiba.
Bw. Faki ametoa kemeo hilo wakati wa mkutano wa dharura ulioitishwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) ili kujadili hali nchini Niger. Akilaani mapinduzi ya hivi majuzi nchini Niger, Bw. Faki alisema hali imevuka hadi mfumo wa Niger kwani itakuwa na athari za kikanda. Hivyo ameonya kuwa kushindwa kusitisha mapinduzi barani Afrika itakuwa ndio kichocheo kikubwa sana cha kuzidisha mabadiliko hayo mabaya ya kikatiba katika bara zima.
Botswana pia ililaani mapinduzi ya Niger mbele ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.