Watu 13 wahofiwa kufariki katika ajali ya boti Ziwa Victoria
2023-08-01 10:13:46| cri

Watu 13 wanahofiwa kufariki dunia huku wengine 14 wakiokolewa baada ya mitumbwi miwili kuzama katika Ziwa Victoria wakati wakitoka kwenye ibada ya Jumapili katika Kijiji cha Ichigondo, Wilaya ya Bunda mkoani Mara, nchini Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema, mwili wa mtoto anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja umeopolewa, na kuongeza kuwa, jitihada za kuwatafuta watu wengine 13 zinaendelea.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.