Benki ya Dunia yaipatia Somalia dola za kimarekani milioni 75 za unafuu wa madeni
2023-08-01 09:39:08| CRI

Benki ya Dunia imesema kuwa imeipatia Somalia ruzuku ya dola milioni 75 ili kuisaidia nchi hiyo kuwa na unafuu wa madeni.

Imesema kuwa serikali inatekeleza mpango kabambe wa mageuzi ya kujenga taasisi, kuvutia uwekezaji, na kufikia ukuaji wa uchumi shirikishi na kuongeza ajira, sambamba na Mpango wa tisa wa Maendeleo wa Taifa unaoainisha maeneo mengi ya kipaumbele ya kuipeleka nchi mbele, ambayo mengi yao yanaungwa mkono na Fedha za Sera ya Maendeleo (DPF).

Meneja wa Benki ya Dunia nchini Somalia Kristina Svensson amesema katika taarifa yake kwamba DPF inaunga mkono matarajio ya serikali ya kujenga misingi ya uchumi wa kisasa wenye taasisi zilizoimarishwa. Pia inaonesha maendeleo makubwa ambayo Somalia imepiga katika suala la ujenzi wa taasisi na maendeleo ya kiuchumi, na kuweka njia kwa ajili ya mustakabali thabiti na endelevu.