Watu wanane wafariki kufuatia mlipuko wa kipindupindu nchini Uganda
2023-08-02 14:41:15| cri

Mkurugenzi wa Afya ya Umma katika Wizara ya Afya nchini Uganda Daniel Kyabanyize amesema, idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa kipindupindu katika maeneo ya katikati na mashariki mwa Uganda imefikia nane.

Amesema mpaka kufikia jana jumanne, idadi ya kesi ilikuwa 25, 10 zilithibitishwa kuwa na ugonjwa huo na 15 zilikuwa zinashukiwa kuwa na maambukizi.

Uganda imethibitisha kuwa na mlipuko wa kipindupindu baada ya watu sita kukutwa na ugonjwa huo katika wilaya ya Kayunga na Namayingo.