Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.6 kwa kipimo cha Richter latokea nchini Eritrea
2023-08-02 08:49:55| CRI

Waziri wa Habari wa Eritrea Yemane Meskel ametangaza kwenye mtandao wa kijamii kwamba tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.6 kwa kipimo cha Richter, na kina cha kilomita 10 limetokea kusini mashariki ya mji mkuu wa Eritrea, Asmara jana jioni.

Nayo Wizara ya Madini na Nishati ya Eritrea, imesema kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Irafalle. Kwa mujibu wa Utafiti wa Kijiolojia wa Marekani, tetemeko hilo la ardhi lilipiga karibu kilomita 55 kusini mashariki ya Asmara. Hadi sasa, hakuna taarifa za uharibifu au majeruhi kutokana na tetemeko hilo.

Asmara, ambayo iko mita zaidi ya 2000 kutoka usawa wa bahari na kuifanya kuwa mji mkuu wa pili kuwa juu zaidi barani Afrika, ilitangazwa kama Eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO kwa usanifu wake wa kisasa uliohifadhiwa vizuri mwaka 2017.