TPDC kuongeza tija uzalishaji gesi
2023-08-03 11:04:49| cri

Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), limeanza kukarabati kisima namba moja cha kuzalisha gesi asilia cha Mnazi Bay, mkoani Mtwara, ili kuongeza tija katika uzalishaji wa umeme nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika la kisima hicho, Meneja wa Uendelezaji na Uzalishaji wa Gesi TPDC, Mhandisi Felix Nanguka, amesema kisima hicho kiligunduliwa mwanzoni mwa mwaka 1982 na kuanza kuzalisha gesi mwaka 2016, na kuongeza kuwa, ukarabati huo unafanyika ili kuongeza uzalishaji kutoka futi za ujazo milioni 10 kwa siku mpaka milioni 17 kwa siku.

Ukarabati wa kisima hicho unafanywa na Kampuni ya Kuzalisha Gesi ya Maurel Prom kwa kuingiza vifaa maalum ndani ya kisima hicho, ili kusaidia kuongeza uzalishaji.