Msemaji wa jeshi la Sudan Nabil Abdalla amesema katika taarifa kwamba vikosi vya Wanajeshi wa Sudan vinakanusha mwelekeo wowote wa kutia saini makubaliano na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), na kubainisha kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamekoma.
Amesema kuwa mazungumzo kuhusu madai ya mapatano si sahihi, na ujumbe wao bado uko nchini na mazungumzo hayo yamesitishwa kwa sasa.
Wiki iliyopita, jeshi la Sudan lilisema ujumbe wake ulirejea nchini kwa ajili ya mashauriano. Habari zimesema kuwa Jumatano jeshi la Sudan na RSF walifanya mashambulizi ya mizinga katika maeneo kadhaa ya Khartoum na Omdurman.
Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya ya Sudan zinaonyesha kuwa Sudan imeshuhudia mapigano makali kati ya pande hizo mbili hasimu mjini Khartoum na maeneo mengine kuanzia Aprili 15, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 na wengine zaidi ya 6,000 kujeruhiwa.