Vikosi vya usalama vya Somalia kwa kushirikiana na wenzi wake wa kimataifa vimewaua wapiganaji zaidi ya 160 wa kundi la al-Shabab katika operesheni ya siku nne iliyofanyika nchini humo.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Utalii wa Somalia Daud Aweis Jama amesema, wapiganaji hao waliuawa katika operesheni tofauti zilizofanyika kuanzia Julai 18 hadi 31 katika mikoa ya HirShabelle na Kusini Magharibi.
Amesema zaidi ya wapiganaji 100 waliuliwa katika mkoa wa Galgaduud, katikati ya Somalia, huku wengine zaidi ya 60 waliuliwa katika operesheni ya kijeshi huko El Dhun, mkoa wa Kusini Magharibi.