Umoja wa Mataifa waonya juu ya kushuka kwa uchumi wa Sudan Kusini
2023-08-03 11:03:32| cri

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMIS) imeonya juu ya kushuka kwa uchumi wa Sudan Kusini wakati mgogoro ukiendelea nchini Sudan.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni kiongozi wa Tume hiyo, Nicholas Haysom amesisitiza kuwa, shambulio katika bomba la mafuta linalosafirisha mafuta kutoka Sudan Kusini kwenda kwenye soko la kimataifa kupitia bandari ya Sudan litadhoofisha uchumi wa Sudan Kusini.

Amesema Umoja wa Mataifa una wasiwasi na hali ya Sudan, na kusisitiza kuwa madhara yake yameiathiri Sudan Kusini, na kuleta ugumu kwa nchi hiyo kukabiliana na masuala muhimu, ikiwemo changamoto za kiuchumi na kibinadamu.