Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imesema, uvamizi wa kijeshi nchini Niger ni uamuzi wa mwisho, kauli ambayo imetolewa wakati Nigeria imekata mgao wa umeme kwa Niger ili kuongeza shinikizo kwa viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini humo.
Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa ECOWAS wamekutana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ili kuandaa majibu ya tukio hilo huku ujumbe mwingine wa Jumuiya hiyo ukienda nchini Niger kwa ajili ya majadiliano, baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini humo.
Ufaransa, ambayo ilitawala Niger, imetuma ndege ya tano kuondoa raia wake nchini humo, wakati kiongozi wa mapinduzi hayo, Jenerali Abdourahmane Tiani akisema hakuna haja ya kufanya hivyo.