UM wasema hali ya njaa na wakimbizi wa ndani inazidi kuwa mbaya nchini Sudan
2023-08-04 12:57:04| cri

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, tatizo la njaa na wakimbizi wa ndani kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Sudan linaendelea kuwa baya nchini humo.

Ofisi hiyo imesema, zaidi ya watu milioni 6 nchini Sudan, ambao ni karibu asilimia 13 ya idadi ya jumla ya watu, wako hatarini kukabiliwa na baa la njaa.

Pia OCHA imesema, zaidi ya watu milioni 20 wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama wa chakula nchini Sudan kutokana na mapigano, kushuka kwa uchumi na idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani.