Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na washirika wake yameomba kutolewa dola za kimarekani bilioni 1.57 kusaidia watu milioni 5.5 katika majimbo matatu yaliyokumbwa na ghasia mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema hadi kufikia katikati ya mwaka huu, mpango wa kukabiliana na misaada ya kibinadamu wa mwaka 2023 nchini DRC wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.3 umefadhiliwa kwa theluthi moja tu.
OCHA imeongeza kuwa fedha hizo zitalenga kutoa msaada wa chakula, lishe, ulinzi na msaada kwa wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia, na pia zitaenda kushughulikia magonjwa ya milipuko katika majimbo haya matatu hadi mwisho wa mwaka.