China yapinga ziara yoyote ya wafarakanishaji wanaotaka "Taiwan Kujitenga na China" kwenda Marekani
2023-08-04 09:58:05| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema China inapinga vikali ziara yoyote ya wafarakanishaji wanaotaka "Taiwan Kujitenga na China" kwenda Marekani kwa jina lolote au kwa kisingizio chochote kile.

Akijibu wanahabari juu ya tangazo lililotolewa na Mamlaka ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (DPP) kwamba naibu kiongozi wa mkoa wa Taiwan Lai Ching-te ataondoka Agosti 12 kwenda Paraguay kushiriki  kwenye sherehe za kuapishwa kwa rais, ambapo njiani pia atapitia   mjini New York na San Francisco nchini Marekani, msemaji huyo amesema China inapinga vikali aina yoyote ya maingiliano rasmi kati ya Marekani na mkoa wa Taiwan, inapinga vikali ziara yoyote ya wafarakanishaji wanaotaka "Taiwan Kujitenga na China" kwenda Marekani kwa jina lolote au kwa kisingizio chochote, na inapinga kithabiti aina yoyote ya uhusiano na uungaji mkono wa Marekani kwa wafarakanishaji wanaotaka "Taiwan  Kujitenga na China" pamoja na shughuli za wasambaratishaji hao.

Amebainisha kuwa swala la Taiwan ni msingi wa maslahi ya China na ni mstari mwekundu ambao hauwezi kuvuka, na kusisitiza kuwa China itafuatilia kwa karibu ziara hiyo na kuchukua hatua kali ili kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi.