Viongozi wa Afrika wasifiwa kwa kuhimiza wanawake na wasichana kufikia uwezo wao
2023-08-07 08:43:20| cri

Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) limewasifu viongozi wa Afrika kwa kuonyesha nia ya kisiasa na uwekezaji unaohitajika ili kuondoa vikwazo vinavyowazuia wanawake na wasichana kufikia uwezo wao.

Mwakilishi wa UNFPA nchini Tanzania Bw. Mark Bryan Schreiner, amesema, wakati idadi ya vijana wanafurahia afya njema, kuendelea na elimu, na wanaweza kuchangia ukuaji wa uchumi, faida ya kiuchumi ya taifa inaweza kuwa kubwa, na mgawanyo wa idadi ya watu unaweza kufikiwa. Hata hivyo, amesema kufikiwa kwa kiwango hiki kunahitaji uwekezaji katika pande nyingi, huku muhimu zaidi ikiwa ni ujenzi wa watu wanaotambua haki zao na kutimiza uwezo wao.

Bw. Schreiner pia amesema, kwa wanawake na wasichana hasa, hii ina maana kuheshimu haki yao ya kutambua uwezo wao wa uzazi, ambao unahitaji kutimiza usawa wa kijinsia.