Rwanda yaadhimisha siku ya mavuno kwa kuimarisha umoja na kuondoa umasikini katika familia
2023-08-07 08:46:26| CRI

Rwanda imesherehekea Siku ya Kitaifa ya Mavuno, kwa lengo la kuwashawishi Wanyarwanda kufanya juhudi ili kuimarisha umoja wa kitaifa, kuondoa umasikini katika familia, na kutimiza ustawi.

Siku hiyo ambayo huadhimishwa ijumaa ya kwanza ya mwezi Agosti kila mwaka, ni ya kitamaduni na ina lengo la kusherehekea mavuno.

Akizungumza katika sherehe hiyo, Waziri wa Kilimo na Rasilimali ya Mifugo nchini humo Idelphonce Musafiri, amesema lengo la kuadhimisha siku hiyo ni kwa ajili ya Wanyarwanda kukusanyika pamoja, kuwasiliana, na kupongezana kwa mafanikio makubwa waliyopata. Pia kuwatia moyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanaweza kudumisha na kujenga mafanikio yao kwa ajili ya siku za baadaye.