Pande hasimu za Sudan zapambana vikali katika mji mkuu
2023-08-07 10:08:34| cri

Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa haraka (RSF) jana vilipambana vikali mjini Khartoum na sehemu nyingine karibu na mji huo kugombea udhibiti wa vituo viwili vya kijeshi kusini mwa Khartoum na Omdurman.

Mapigano hayo yamesababisha kukatika kwa mawasiliano na huduma ya Internet kwa masaa mengi katika eneo la mji mkuu kuanzia alfajiri ya jana. Wakazi wenyeji wamesema pande hizo mbili zote zimeweka amri ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi na mbili alfajiri katika maeneo zinayodhibiti.

Mgogoro huo nchini Sudan ulianzia mjini Khartoum Aprili 15 na sasa umeenea na kuathiri maeneo mengine ya nchi hiyo.