Rais wa Nigeria azindua mradi wa ujenzi wa kituo cha umeme unaojengwa na kampuni ya China
2023-08-07 08:45:44| CRI

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha umeme wa gesi unaofanywa na kampuni Uhandisi wa Mashine ya China.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, rais Tinubu amesema mradi huo ni muhimu sana kwa Nigeria, na pia ni hatua ya kwanza katika juhudi za serikali za kuanzisha sekta yenye nguvu ya nishati ambayo itachochea ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

Naye Balozi wa China nchini Nigeria, Cui Jianchun, ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua, kuwa mradi huo utachukua nafasi muhimu katika kuisaidia Nigeria kuondokana na pengo la upatikanaji wa umeme. Ameongeza kuwa, utakapokamilika, mradi huo unatarajiwa kukabiliana na mahitaji ya umeme kwa mji mkuu wa Nigeria na maeneo ya jirani.