Zaidi ya wanadiplomasia 40 na wawakilishi wa serikali kutoka Asia, Amerika Kusini na Afrika wajionea wenyewe mkoa unaojiendesha wa Xinjiang
2023-08-08 08:37:32| CRI

Zaidi ya wanadiplomasia 40 na wawakilishi wa serikali kutoka Asia, Amerika Kusini na Afrika wametembelea mradi wa maji na mashamba ya matunda katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang kaskazini mashariki mwa China kujifunza namna mkoa huo umefanikiwa kiamendeleo licha sehemu kubwa kuwa jangwa na milima. Wanadiplomasia hao wameipongeza Xinjian na China kwa jumla kwa jitahada zake za kufanikisha maendeleo ya kisasa.