WHO yaimarisha hatua ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Somalia
2023-08-09 08:38:09| cri

Shirika la Afya Duniani (WHO) jana limesema, limeimarisha hatua ili kuokoa maisha na kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Somalia baada ya watu 30 kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo tangu mwezi Januari.

Shirika hilo limesema, ugonjwa wa kipindupindu umeenea kwenye mikoa 28 iliyokumbwa na ukame tangu mwaka 2022 na kwenye mkoa wa Banadir tangu kutokea kwa ukame mwaka 2017.

Shirika hilo pia limesema, tangu mwanzoni mwa mwaka 2023, jumla ya kesi 11,704 za kipindupindu ikiwa ni pamoja na vifo vya watu 30 viliripotiwa katika mikoa 28 nchini Somalia.