Michezo ya 31 ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Joto yamalizika kwa mafanikio huko Chengdu
2023-08-09 08:38:05| cri

Michezo ya 31 ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Joto imemalizika kwa mafanikio jana jioni huko Chengdu, Mkoa wa Sichuan, China.

Katika siku 12 zilizopita, wanariadha 6,500 kutoka nchi na sehemu 113 wameonesha sura mpya ya mshikamano na urafiki. China,  inayofuata dhana ya mashindano rahisi, salama na ya kusisimua, imesifiwa na Shirikisho la Michezo ya Vyuo Vikuu na jumuiya ya kimataifa.

Wanariadha wa China walishinda medali 103 za dhahabu na medali 178 katika michezo hiyo, wakishika nafasi ya kwanza katika orodha ya medali za dhahabu na orodha ya medali.