Mapigano makali yaendelea huko Omdurman nchini Sudan na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20
2023-08-09 10:33:43| cri

Idara ya afya ya jimbo la Khartoum nchini Sudan imetoa taarifa kupitia vyombo vya habari vya kijamii ikisema mapigano makali yametokea mjini Omdurman, kaskazini magharibi mwa mji wa Khartoum, ambako baadhi ya maeneo ya makazi ya watu yalishambuliwa kwa mizinga, na kusababisha vifo vya raia zaidi ya 20 na wengine wengi wamejeruhiwa.

Idara hiyo pia imesema akiba ya damu kwenye hospitali moja tu inayoendelea kutoa huduma mjini Omdurman imekwisha, na kutoa wito kwa watu kuchangia damu kwenye hospitali hiyo.

Hivi karibuni mapigano yamekuwa yakipamba moto eneo la Khartoum Kaskazini na Omdurman, na kusababisha vifo na majeruhi ya raia, na kuwafanya raia wengi wakimbie makazi yao.