China yachukua nafasi ya kwanza kwenye sekta ya uuzaji wa magari nje
2023-08-09 10:34:13| cri

Takwimu za biashara ya nje kutoka Idara kuu ya forodha  ya China zinaonesha kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi Julai mwaka huu, thamani ya uuzaji wa mashine na vifaa vya umeme nje ya nchi, haswa magari, imeongezeka hadi asilimia 58.1 ya jumla ya uuzaji nje wa bidhaa.

China iliizidi Japan kwa uuzaji wa magari nje katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka, na pia katika nusu ya kwanza ya mwaka huu na hivyo kuchukua nafasi ya kwanza duniani. China imekuwa nchi inayozalisha magari kwa wingi, inayotumia magari kwa wingi na inayouza magari kwa wingi. Takwimu pia zinaonesha kuwa kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu, China imeuza magari milioni 2.778 nje ya nchi, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 74.1 ikilinganishwa na mwaka jana, na thamani yake imekuwa yuan bilioni 383.73 (sawa na dola bilioni 53.2 za kimarekani), kiasi ambacho kimeongezeka kwa asilimia 118.5.