Miji 30 ya Afrika yenye akili kutambuliwa katika mkutano wa Kigali
2023-08-10 22:31:54| cri

Walau miji 30 ya Afrika inatarajiwa kutambuliwa kama miji yenye masuluhisho ya teknolojia za kisasa, wakati wa mkutano ujao wa uwekezaji kwenye miji endelevu na yenye akili utakaofanyika kuanzia Septemba 6-8 mjini Kigali.

Mkutano huo utakaowajumuisha washiriki 1,000, unalenga kuhimiza ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, kuonyesha njia za ufumbuzi kwenye miji inayotumia teknolojia za kisasa, na kutambua fursa za uwekezaji zinazoweza kupatikana kwenye miji endelevu na inayostawi ya Afrika.

Msimamizi Mkuu wa mkutano huo Bw. Jean-Philbert Nsengimana, amesema mabadiliko hayo yataangalia masuluhisho kama vile usambazaji wa nishati endelevu, nyumba za bei nafuu, teknolojia na vifaa vya ujenzi, usafiri na upatikanaji wa huduma za mijini, kukabiliana na msongamano wa magari, uchafuzi wa mazingira na majengo yanayotumia nishati mpya.