Maofisa wa Madagascar wasema maonesho ya biashara kati ya China na Afrika ni fursa adimu ya kuonyesha na kutangaza bidhaa za Afrika
2023-08-10 08:38:31| CRI

Maofisa kutoka nchini Madagascar wamesema, Maonesho ya Tatu ya Biashara na Uchumi kati ya China na Afrika yamekuwa jukwaa bora na fursa adimu ya kutangaza bidhaa kutoka Madagascar na nchi nyingine za Afrika, na kutoa mchango mkubwa katika ustawi wa pamoja.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Uhusiano na Diaspora iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Madagascar, Emi-Haulain Kola amesema, maonyesho hayo yalihudhuriwa na wafanyabiashara kutoka nchini humo, ambao walipata fursa ya kuonyesha bidhaa maarufu za Madagascar.

Madagascar ilikuwa moja ya nchi wageni wa heshima katika Maonesho hayo, na kampuni saba kutoka nchini humo zilionyesha bidhaa mbalimbali ikiwemo vanilla, karafuu, chocolate na mafuta muhimu pamoja na mvinyo.

Kando na maonesho hayo, China na Madagascar zilisaini makubaliano kuhusu ukaguzi na karantini kwa nyama ya kondoo kutoka Madagascar inayosafirishwa katika soko la China.