Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama--“mama waliobeba maziwa”
2023-08-11 08:00:46| CRI

Kuanzia Agosti Mosi hadi 7, dunia huadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama. Katika kipindi cha wiki iliyopita, tumeshazungumzia haki za mwanamke mwajiriwa katika kunyonyesha pindi anapojifungua. Kutokana na maendeleo ya jamii, wanawake wengi zaidi wanafanya kazi nje tofauti na vizazi vilivyopita, na wanatakiwa kurudi kazini pindi likizo ya uzazi inapomalizika, na hivyo kupunguza muda wa kuwanyonyesha watoto wao wachanga. 

Nchini China kuna wanawake wanaitwa “mama waliobeba maziwa”, na hii ni kutokana na kwamba, wanabeba vifaa maalum vya kukamulia maziwa wanapokuwa maofisini, na wanaporudi nyumbani, wanayahifadhi ili watoto wao waweze kunywa siku inayofuata. Katika kipindi chetu cha leo cha Ukumbi wa Wanawake tutaendelea kuangazia umuhimu wa maziwa ya mama na haki ya mama mwajiriwa anayenyonyesha.