DRC kuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi tatu kuhusu misitu ya kitropiki duniani
2023-08-11 08:37:01| CRI

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa kwanza wa pande tatu kuhusu uhifadhi wa misitu ya kitropiki duniani, ikiwa pamoja na nchi za Brazil na Indonesia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya DRC, Mkutano huo utafanyika mjini Kinshasa tarehe 25 mwezi huu, na utawakutanisha rais wa DRC Felix Tshisekedi, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, na Rais wa Indonesia Joko Widodo.

Mkutano huo utazingatia zaidi eneo la Bonde la Kongo linalochukua zaidi ya asilimia 60 ya ardhi ya DRC ambalo linajulikama kama “mapafu ya Afrika” na kuvuta kiasi kikubwa zaidi cha kaboni duniani. Msitu huo unafunika nchi sita duniani, ni chanzo cha usalama wa chakula na maisha muhimu kwa watu wa asili na wenyeji wa huko, na umekuwa makazi muhimu kwa spishi zilizo hatarini.