ECOWAS yatangaza kuanzisha kikosi cha kikanda kukabiliana na mgogoro wa Niger
2023-08-11 08:33:23| cri

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) jana walifanya mkutano wa dharura huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria, wakitangaza kuanzishwa mara moja kwa kikosi cha kikanda ili kukabiliana na mgogoro wa Niger.

Taarifa iliyotolewa na ECOWAS imesema, Jumuiya hiyo itaendelea kujitolea kutatua mgogoro unaoikabili Niger kwa njia ya amani, na kuweka vikwazo kwa watu binafsi na mashirika yote yanayozuia Niger kurejesha utaratibu wa kikatiba. Pia imetoa wito kwa Umoja wa Afrika na jumuiya ya kimataifa kuunga mkono maamuzi ya ECOWAS.