Mkurugenzi mkuu wa Kituo cha Kusini, Carlos Maria Correa, amesema mkutano wa kilele wa 15 wa BRICS utakaofanyika nchini Afrika Kusini mwezi huu, unatarajiwa kuufanya utaratibu wa uongozi wa dunia kuwa wa haki zaidi na kukabiliana na umwamba wa nchi za Magharibi.
Amesema ajenda kuu za mkutano huo zitajikita katika juhudi za kuacha matumizi ya dola na hivyo kupunguza nguvu ya dola duniani, na upanuzi wa Kundi hilo kwa kuongeza wanachama wapya, na pia kujadili kigezo cha kuwa wanachama na mwongozo wa kanuni.
Mpaka sasa, nchi 20 zimewasilisha maombi rasmi kuwa wanachama wapya wa BRICS, ambazo ni pamoja na Saudi Arabia, Iran, Falme za Kiarabu, Argentina, Indonesia, Misri na Ethiopia.