Rais wa Uganda asikitishwa na Benki ya Dunia kusitisha ufadhili kwa Uganda
2023-08-11 08:34:15| CRI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameilaani Benki ya Dunia kwa kusitisha ufadhili mpya kwa nchi hiyo kufuatia sheria ya kuwaadhibu watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Rais Museveni amesema, bila hata ya ufadhili wa Benki hiyo, nchi yake itaendelea kupata maendeleo, na kuongeza kuwa, kuna vyanzo vingine vingi vya ufadhili ambavyo Uganda inaweza kukopa kutoka kwao.

Rais Museveni amesema, kwa kutumia nidhamu, uzalendo na kupambana na rushwa, nchi hiyo itastawi kwa kuwa sekta ya kilimo inaendelea vizuri, viwanda vinakua na sekta ya huduma nchini humo pia inapanuka.