Kikundi cha madaktari wa China nchini Algeria chawatibu wagonjwa zaidi ya milioni 27 kwa ujumla katika miaka 60 iliyopita
2023-08-11 15:37:04| cri

Huu ni mwaka wa 60 tangu China ilipotuma vikundi vya madaktari nchi za nje. Tangu China ilipotuma kikundi cha kwanza cha madaktari nchini Algeria mwaka 1963, vikundi vya madaktari vya China katika nchi za nje vimewatibu wagonjwa takriban milioni 300 kwa jumla. Katika miaka hiyo 60, vikundi vya madaktari vya China vimetoa huduma katika nchi na sehemu nyingi zinazoendelea za Asia, Afrika na Latin Amerika.

Mwezi Aprili mwaka 1963, serikali ya China ilijibu kwa makini wito wa dharura uliotolewa na serikali ya Algeria, na kutuma kikundi chake cha kwanza cha madaktari nchini humo. Hadi sasa China imetuma vikundi 27 vya madaktari nchini Algeria vyenye wahudumu wa afya 3,522, ambao wamewatibu wagonjwa zaidi ya milioni 27 kwa ujumla, na kuwasaidia wajawazito kujifungua watoto zaidi ya milioni 2.07. Ustadi wa madaktari wa China umesifiwa sana na watu wa huko.