Wanafunzi 48 wa Kenya kuanza masomo yao ya elimu ya juu nchini China
2023-08-11 08:34:58| CRI

Ubalozi wa China nchini Kenya jana alhamis ulifanya sherehe ya kuwaaga wanafunzi 48 waliopata ufadhili wa kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu nchini China kupitia Ufadhili wa Serikali ya China kwa mwaka 2023.

Wanafunzi hao wanatarajiwa kuondoka nchini Kenya wiki ijayo ili kuendelea na masomo yao nchini China katika fani mbalimbali ikiwemo utawala, uhandisi, uhusiano wa kimataifa na lugha ya Kichina katika ngazi za diploma na shahada za juu.

Tangu mwaka 1982, serikali ya China imekuwa ikitoa ufadhili kwa maelfu ya wanafunzi kutoka nchini Kenya.