Russia kutoa tani 25,000 hadi 50,000 za nafaka bila malipo kwa nchi 6 za Afrika
2023-08-11 11:05:29| cri

Waziri wa kilimo wa Russia Bw. Dmitry Patrushev amesema Russia itatoa bure tani 25,000 hadi 50,000 za nafaka kwa nchi 6 za Afrika katika siku za karibuni.

Bw. Patrushev amesema mwaka huu wa fedha, Russia iliuza tani milioni 60 za nafaka kwa nchi za nje, na katika mwaka ujao wa fedha mauzo ya nafaka kwa nchi za nje yanatarajiwa kufikia tani milioni 55. Amesisitiza kuwa ikiwa ni nchi rafiki, Russia daima itakuwa mshirika wa kuaminika katika suala la utoaji wa chakula.