Uganda imerejesha matumizi ya vifaa vya kupima ulevi barabarani ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuzuia ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva walevi.
Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ya Uganda imesema uamuzi wa kurejesha vifaa hivyo umefikiwa baada ya kuchambua vyanzo vya ajali za barabarani. Wizara hiyo imesema waganda ndio watumiaji wakuu wa pombe barani Afrika, na wengi huendesha magari wakiwa wamekunywa pombe.
Utumiaji wa vifaa hivyo ulisitishwa mwaka 2020 baada ya kuzuka kwa janga la COVID-19, na tangu kusitishwa huko Uganda imesajili ongezeko kubwa la ajali za barabarani huku asilimia 40 zikisababisha vifo.