Shirika la habari la MAP limeripoti kuwa jeshi la majini la Morocco limewaokoa wahamiaji 130 wa Senegal katika pwani ya Atlantiki karibu na mji wa Dakhla.
Kikosi cha doria cha jeshi la majini la Morocco kiliizuia boti moja iliyokuwa inasafiri kutoka bandari ya Fass Boye huko Senegal kuelekea kaskazini kwenye visiwa vya Canary vya Hispania katika bahari ya Atlantiki.
Pia siku ya Jumapili, kikosi cha uokoaji cha visiwa vya Canary kilitangaza kukamata boti moja ya mpira na kuwaokoa watu 53 waliokuwa kwenye boti hiyo karibu na pwani ya Fuerteventura.