UAE yakanusha kutoa silaha kwa pande zinazopigana nchini Sudan
2023-08-14 08:46:28| CRI

Umoja wa Falme za Kiarabu imekanusha madai kwamba imetoa silaha kwa pande zinazopigana nchini Sudan.

Shirika la serikali la nchi hiyo WAM limemnukuu ofisa wa wizara ya mambo ya nje Bi. Afra Al Hameli akisema UAE haitachagua upande wa kuuunga mkono katika mgogoro wa Sudan, na inatoa wito wa kuheshimiwa kwa mamlaka ya Sudan na kupatikana kwa njia ya kutatua mgogoro.

Ofisa huyu ametoa kauli hiyo baada ya Jarida la Wall Street kuripoti wiki iliyopita kwamba masanduku ya silaha yaligunduliwa mwezi Juni kwenye ndege moja ya mizigo kutoka UAE iliyokwenda Uganda, badala ya msaada kwa wakimbizi wa Sudan kama ilivyoonyeshwa kwenye rekodi za ndege.