Watu 89 wafariki kutokana na moto wa msituni huko Hawaii nchini Marekani
2023-08-14 11:08:26| cri

Mkuu wa jimbo la Hawaii Bw. Josh Green Jumamosi alisema idadi ya watu waliofariki kutokana na moto wa msituni uliotokea katika kisiwa cha Maui jimboni Hawaii nchini Marekani imeongezeka hadi 89.

Moto huo umefanya kuwa ni ajali iliyosababisha vifo vya watu wengi zaidi nchini Marekani katika karne zaidi ya moja iliyopita, ambapo idadi ya vifo vya watu imezidi ile ya ajali ya moto ya kambi iliyotokea tarehe 8 Novemba mwaka 2018 jimboni California na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 85.

Kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Jumatano iliyopita Green alionya kuwa idadi ya vifo vya watu inaweza kuendelea kuongezeka, akisema serikali imezipatia familia zilizopoteza makazi vyumba 1,500.