Watumiaji wa ziwa Victoria kupata vituo vya uokoaji
2023-08-15 14:00:06| cri

Tume ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC), pamoja na serikali ya Uganda, wameanza kujenga vituo vya uokoaji katika ziwa hilo ili kuokoa maisha ya wasafiri.

Hatua hiyo imekuja baada ya watu 17 kuthibitishwa kufa maji na wengine kadhaa wakiwa wamezama na bado hawajapatikana, kufuatia ajali ya boti. Maafisa wa Tume ya Bonde la Ziwa Victoria, ambao mwishoni mwa wiki walitoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na majaketi na vyakula kwa familia za wahanga, walisema vituo vya uokoaji vitarahisisha kukabiliana na dharura ziwani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Bonde la Ziwa Victoria, Dk Masinde Bwire alisema kama taasisi inayoratibu nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ina nia ya dhati ya kutoa usafiri wa majini ulio salama katika Ziwa Victoria.