Mkutano wa ushirikiano wa vyombo vya habari wa “Washirika wa Afrika” 2023 wafanyika Nairobi
2023-08-15 13:56:29| cri

Chini ya kaulimbiu ya “Kutafuta kujifunza kwa pamoja kati ya ustaarabu tofauti na kujenga mustakabali kwa ushirikiano”, Mkutano wa ushirikiano wa vyombo vya habari wa “Washirika wa Afrika” 2023 ulioandaliwa kwa pamoja na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na Umoja wa Watangazaji Barani Afrika (AUB) umefanyika tarehe 14 mwezi huu huko Nairobi, Kenya.

Naibu mkurugenzi wa Idara ya utangazaji ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisiti cha China (CPC), ambaye pia ni Waziri wa Utamaduni na Utalii Bw. Hu Heping akihutubia mkutano huo alisema, wakati Rais Xi Jinping alipofanya ziara barani Afrika mwezi Machi mwaka 2013 alitoa nadharia muhimu kwa mara ya kwanza kuwa “China na Afrika siku zote ni jumuiya yenye mustakabali wa pamoja”, pamoja na dhana ya ukweli, uhalisi, karibu na udhati, na wazo sahihi la kufuata maadili na kuzingatia maslahi. Pia amesema katika muongo mmoja uliopita, pande hizo mbili zimekuwa zikidumisha urafiki wa dhati, kutendeana kwa usawa, na kuwa na ushirikiano wa kunufaishana. Hayo yote yamefanya wazo la Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya kuwa na mambo mengi zaidi na malengo  na njia wazi zaidi. Mwezi Machi mwaka huu, kufuatia Pendekezo la Maendeleo ya Kimataifa na Pendekezo la Usalama wa Kimataifa, Rais Xi Jinping kwa mara ya kwanza alitoa Pendekezo la Ustaarabu la Kimataifa likitoa wito wa kuheshimu ustaarabu anuwai duniani, kueneza thamani ya pamoja ya binadamu wote, kuzingatia urithi na uvumbuzi wa utamaduni, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa utamaduni duniani, na kujadiliana juu ya ujenzi wa mtandao wa mazungumzo na ushirikiano kati ya ustaarabu tofauti duniani. Mkutano huo una umuhimu mkubwa katika kuhimiza sekta mbalimbali kupanga ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika kwa upeo mpana zaidi, na kujenga Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya.

Naibu mkurugenzi wa Idara ya Utangazaji ya Kamati Kuu ya CPC na Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong akihutubia mkutano huo kwa njia ya video ametoa wito kwa vyombo vya habari vya China na Afrika kushirikiana kujenga upya mazingira ya vyombo vya habari duniani, kuhimiza mawasiliano kati ya ustaarabu wa China na Afrika, ili kuufanya ustaarabu tofauti duniani uoneshe uzuri na uhai wao. Amesisitiza kuwa CMG inapenda kushirikiana na washirika wake wa Afrika, kuchangia busara na nguvu katika kukuza ujenzi wa Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya

Mkurugenzi mtendaji wa AUB Bw. Grégoire Ndjaka amesema utamaduni wenye utajiri na uhai mkubwa umeundwa katika historia ya utamaduni ya China ya zaidi ya miaka 5000, ambayo inachangia sana katika ujenzi wa ustaarabu wa kisasa wa taifa la China. Amesema Rais Xi Jinping aliwahi kusisitiza kuwa, inapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu ustaarabu wa China, na kwamba Afrika pia inajitahidi kueleza hadithi zake za kweli. Bw. Ndjaka amesisitiza kuwa wako tayari kushirikiana na CMG kuhimiza watu wa pande mbili kuelewana na maendeleo ya kijamii.  

Awamu ya Pili ya shughuli ya Kukusanya Video Fupi za vijana wa China na Afrika iliyoandaliwa na Kituo Kikuu cha Afrika cha CMG imezinduliwa rasmi katika mkutano huo. Lengo la shughuli hizo ni kukusanya kwa wingi zaidi video fupi bora, ili kuufanya urafiki kati ya China na Afrika uoneshwe kwa kutosha kupitia kamera.  

Azimio la Pamoja la Ushirikiano la Vyombo vya Habari la 2023 limetolewa katika mkutano huo. Azimio hilo lililozinduliwa kwa pamoja na CMG na AUB linalenga kukuza ushirikiano kati ya vyombo vya habari na kusimulia vizuri hadithi za China na Afrika, kuimarisha ushirikiano na mshikamano, kulinda usawa na haki, na kushikilia uvumbuzi ili kuimarisha matumizi ya teknolojia.