Maelfu ya kampuni zafungwa kufuatia hali ngumu nchini Kenya
2023-08-15 08:56:16| cri

Kampuni 9,441 zilizosajiliwa zimefungwa rasmi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita huku idadi kubwa zikilazimika kusitisha shughuli zake kutokana na nyakati ngumu pamoja na mazingira magumu ya kuendesha biashara.

Hata hivyo, baadhi ya kampuni zilikuwa biashara za muda mfupi tu zilizoanzishwa kwa kusudi fulani kama vile kugombea zabuni za mamilioni na kisha kufunganya virago baada ya kutimiza kusudi zake.

Takwimu kutoka Idara ya Usajili wa Biashara (BRS) zinaashiria kuwa mashirika 2,030 yalifutiliwa mbali na Msajili wa Kampuni kwenye bajeti iliyokamilika 2022/23 idadi iliyoongeza kampuni 2,189 zilizofungwa mwaka uliotangulia.