Timu ya madaktari ya China yatoa mhadhara kuhusu Tiba ya Jadi ya Kichina kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Namibia
2023-08-15 08:34:24| CRI

Timu ya madaktari ya China nchini Namibia jana Jumatatu ilitoa mhadhara kuhusu Tiba ya Jadi ya Kichina (TCM) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Namibia, ili kuwawezesha kupata uelewa mzuri kuhusu TCM.

Kwenye mhadhara huo uliofanyika katika Taasisi ya Confucius ya chuo kikuu hicho, madaktari wa China walifafanua kwa kina kuhusu Tiba ya Jadi ya Kichina, ikiwa ni hatua inayolenga kutoa ujuzi na kuwaelimisha zaidi wanafunzi kuhusu manufaa ya tiba hiyo ambayo ni mbadala wa matibabu mengine ya kisasa.